Nafasi ya Kazi, Halmashauri ya Wilaya ya Hai – Dereva

Spread the love

Nafasi ya Kazi, Halmashauri ya Wilaya ya Hai – Dereva

Kumb.Na.LG/S.10/01/142 Tarehe: 12/02/2024

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anawatangazia watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA.228/613/01/022 cha tarehe 08.12.2023 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.

1.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 1)

1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV)

Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.

1.2.2 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;

iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na vi. Kufanya usafi wa gari.

1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA

Ngazi ya Mshahara ni TGS B

MASHARTI YA UJUMLA

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

iii. Waombaji ambao ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi waUmma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 25 Februari, 2024.

xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI,
S.L.P 27,
HAI.

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Limetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA KAZI HII