Nafasi 2 za Kazi, Shule ya St Jude – Udereva

Spread the love

Nafasi 2 za Kazi, Shule ya St Jude – Udereva

Tangazo la Kazi: Nafasi za Udereva (2)

Kuhusu Shule

Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude’s inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora.

Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi mbili (2) za kazi ya Udereva kwa watanzania wenye sifa stahiki.

Kazi na Majukumu

  • Kuendesha magari ya shule kwa uangalifu na umakini
  • Kuwa makini na kukagua wa mara kwa mara gari ulilokabidihiwa kuhakikisha lipo salama kabla ya na wakati wa kuliendesha
  • Kutunza taarifa za gari/vipuri/mafuta na mabadiliko yoyote ikiwemo kujaza “log book” kwa usahihi na kwa kila tukio na safari za gari
  • Kuripoti kwa wakati muda wa gari kukarabatiwa na/au kwenda “service”
  • Kufuata taratibu sheria kanuni na miongozo ya usalama barabarani
  • Kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya shule na taasisi husika pale linapotokea tatizo kwa gari la shule unaloendesha
  • Kufuata mipangilio na ratiba za magari na maelekezo ya Dereva Mkuu kuhusu Route za magari
  • Kushiriki sikukuu na shughuli za kijamii za The School of St. Jude mara zipangwapo
  • Kutoa taarifa ya maandishi ikiwa gari unaloendesha litapata hitilafu au ajali itakayozuia safari iliyopangwa au ruti kuendelea.

Sifa za Mwombaji

  • Mwombaji ajue kusoma na kuandika
  • Mwombaji awe na Cheti cha Udereva kutoka kwenye chuo kinachotambulika
  • Mwombaji awe na leseni hai ya daraja “C”
  • Awe na uzoefu wa angalau miaka mitatu (3) ya kuendesha magari ya shule.
  • Mwombaji awe Mtanzania mwenye kitambulisho cha Taifa

Faida ya ziada

  • Ana cheti cha kuthibitisha ujuzi wa Kiingereza

Ujuzi wa kutumia kompyuta

Vigezo na Masharti

Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu

  • Aambatanishe barua ya uhakiki wa leseni kutoka polisi.
  • Aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa na Maelezo binafsi (CV)
  • Aambatanishe barua kutoka kwa mtendaji au mwenyekiti wa mtaa
  • Aambatanishe barua kutoka kwa muajiri aliepita
  • Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Moshono Kampasi kabla au mnamo Ijumaa, tarehe 23 Februari 2024. Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.

TUTAWASILIANA NA WALE WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAHOJIANO!

ANGALIZO:

TAFADHALI KUWA MAKINI NA MATENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI.