Hakuna kipa aliyehusika kwenye ufungaji zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza [ bao 1 & asisti 4 ].

Rekodi ya Alisson Becker Kwenye Ligi kuu ya Uingereza:-

  • Kipa pekee aliyefunga bao la ushindi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza
  • Kutoa asisti ya Mabao ya Mohamed Salah dhidi ya Manchester United na Manchester City
  • Gloves 2 za Dhahabu katika misimu 4 ya Ligi Kuu

Alisson Becker. Mlinda mlango kamili zaidi katika historia ya Ligi Kuu

Soma pia: Ratiba ya Kombe la Dunia 2022 | FIFA World Cup Qatar 2022 schedule

Alisson aliyesajiliwa na Liverpool kutoka Roma ya Italia, katika msimu wa joto wa 2018 kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa pauni milioni 66.8. Alisson ameonekana kuinuliwa zaidi na Liverpool. Maisha ya soka ya Alisson yamekuwa tofauti kabisa na ya Goalkipa Kepa Arrizabalaga pia wa ligi Kuu Uingereza, ambaye Chelsea ilivunja rekodi hiyo ya uhamisho kumsajili wiki chache baadaye na ambaye amekuwa akipata tabu sana Uwanjani tangu kuhama kwake, hali hii inaangazia ni kiasi gani cha mafanikio ambacho Alisson amekuwa nacho. Katika misimu yake miwili ya kwanza Anfield, Alisson alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Uingereza / Premier League, Kombe la Super ‘Cup’ la Ulaya na Kombe la Dunia la Vilabu, huku Liverpool FC ya Jürgen Klopp ikikua na kuwa moja ya timu kubwa na bora zaidi za nyakati za sasa kwenye Ulimwengu wa Soka.