Meta Kampuni Mama ya WhatsApp wametoa sasisho jipya lenye maboresho zaidi. Kuanzia sasa watumiaji wa WhatsApp watakutana na kitu kinachoitwa WhatsApp Community kupitia akaunti zao za App ya WhatsApp.

Meta wameachia sasisho jipya liitwalo WhatsApp community ambayo linafanya kazi ya kuunganisha zaidi ya groups 21 kuwa kitu kimoja.

Zamani ilikua kumuingiza mtu kwenye Group la WhatsApp mpaka uwe na namba yake au uwatumie link, ila Sasa kupitia Whatsapp Community utakua na uwezo wa kuwakutanisha watu zaid ya 10000+ kuwa kitu kimoja.

Hivyo kwa sasa utaweza kujumuisha zaidi ya magroup 50 kuwa group Moja na watu kuwafanya kuwa pamoja wataweza kuchati , kupiga simu na kadhalika.

Kwenye Whatsapp Community namba za simu za watu zitakua zinafichwa na hutaweza kuona namba ya mtu yeyote yule isipokuwa ya admin tu na wale ambao uko nao kwenye group Moja.

Whatsapp Community inawezesha kuunganisha watu ulimwenguni kupitia Intaneti kutoka mawasiliano ya mmoja kwa mmoja, kuwa mawasiliano ya kijamii zaidi kupitia WhatsApp.

Meta yatoa sasisho Jipya liitwalo ‘WhatsApp Community’

Ingizo hili Jipya la WhatsApp litawezesha mambo yafuatayo :-

• Admin akituma tangazo litaweza kuonekana kwa watu wote
• Admin atakua na uwezo wa kufuta message ya mtu yeyote
• Ukijitoa kwenye Whatsapp community hakuna atakayejua kuwa umejitoa.
• Utakua na uwezo wa kuunganisha watu zaidi ya 32 kwenye ‘Group call’ Moja na kadhalika.

Kuona ingizo / feature hii mpya, fanya update kwenye Whatsapp yako na utaona Kuna logo ya watu wengi wako pamoja karibu na chati.

Kumbuka: Communities kwenye WhatsApp zinapatikana katika nchi chache na huenda zisipatikane kwako kwa wakati huu.
Communities zimeanza kutolewa na Meta na zitapatikana kwa watumiaji kote ulimwenguni hivi karibuni.