Tangazo la Nafasi 2 za Kazi , Halmashauri ya Wilaya Muleba – Dereva Mashua / Vivuko Daraja II – Mei 2025.
HALMASHAURI YA WILAYA MULEBA
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. KGR/ML/HW/A.225/VOL.V/83 Tarehe: 20/05/2025
Yah: TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amepokea kibali cha Ajira kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo;-
1.0 DEREVA MASHUA/VIVUKO DARAJA II – NAFASI 2
1.1 KAZI/MAJUKUMU
i. Kufunga na kufungua kamba za Mashua / Kivuko
ii. Kuchunga usalama wa abiria na Magari yaliyomo ndani ya Mashua/Vivuko iii. Kupanga abiria au magari kwenye mashua/Kivuko
iv. Kuendesha na kuongoza Mashua/kivuko
v. Kutunza daftari za safari ya Mashua/Kivuko
vi. Kuhakikisha kwamba injini za Kivuko zipo katika Hali nzuri ya kufanya kazi vii. Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi
1.1.1 SIFA ZA MUOMBAJI
i. Awe na Elimu ya kidato cha NNE (IV)
ii. Awe na ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute na Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka mawili
iii. Awe na amefaulu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA TGOS A
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iii. Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na kuhitimu mafunzo ya Kitaaluma. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
iv. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
v. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
vi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
vii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 3 Juni, 2025.
viii. MUHIMU. Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ya; –
MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA MULEBA, S.L.P 131, MULEBA
ix. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xi. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MULEBA
Nafasi 2 za Kazi , Halmashauri ya Wilaya Muleba – Dereva Mashua / Vivuko Daraja II – Mei 2025 :-
Bofya Hapa Kutuma Maombi Yako Kupitia Ajira Portal
Soma Pia: Nafasi 100 za Kazi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) – Ajira Mbalimbali