Nafasi 2 za Kazi za Mpishi – Shule ya St Jude

Spread the love

Soma hapa taarifa kuhusu Nafasi 2 za Kazi za Mpishi – Shule ya St Jude

Tangazo la Kazi: Nafasi ya Mpishi (2)

Kuhusu Shule

Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude’s inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora.

Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi ya kazi ya mfanya usafi kwa watanzania wenye sifa stahiki.

Kazi na Majukumu

–       Kuandaa chai, uji, matunda na chakula cha mchana cha wanafunzi na wafanyakazi kama mboga, wali, maharage, nyama na vyakula vingine kulingana na ratiba ya chakula elekezi.

–       Kupakua chakula kwenye vyombo yaani madishi, ndoo, treyi na kukabidhi kwa viongozi wa meza wa wanafunzi.

–       Kutoa taarifa kwa mwalimu au mfanyakazi wa zamu ikiwa wanafunzi wameacha bwalo au vyombo vikiwa vichafu.

–       Kuweka vyombo na vifaa vingine vitumikavyo jikoni katika hali nzuri na ya usafi wakati wote.

–       Kuhakikisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wanaosaidia kazi jikoni.

–       Kushirikiana na mpishi mkuu/msaidizi wake kuhakikisha mtu yeyote au mwanafunzi asiyehusika haingii jikoni.

–       Kuwasimamia viongozi wa chakula wa wanafunzi jikoni kwa ushirikiano na mwalimu/mfanyakazi wa zamu.

–       Kuhakikisha chakula kimechambuliwa na ni kisafi kabla ya kupika. Mf: Maharage, mchele, mboga.

–       Kuhakikisha vyombo ni visafi jikoni na viwe katika mpangilio mzuri wakati wote.

–       Kuhakikisha unatunza vyombo na vifaa vingine jikoni na uharibifu au upotevu unapotokea toa taarifa mapema angalau ndani ya masaa 24.

–       Kuhakikisha unatoa chakula kwa wanafunzi kwa utaratibu na muda uliopangwa na uongozi wa shule. Usitoe chakula au vitu vingine vya kula kwa mwafunzi yeyote nje ya utaratibu au bila ruhusa toka kwa kiongozi wako.

Sifa za Mwombaji

–          Mwombaji awe na uwezo wa Kupika vizuri kwa kufuata kanuni za Afya

–          Mwombaji awe na uzoefu wa kupika kwenye mashule na taasisi mbalimbali angalau miaka isiyo pungua Mitatu.

–          Mwomabaji awe na cheti cha upishi kutuko chuo au taasisi inayotambulika na Serekali

–          Mwombaji awe anaishi mazingira ya karibu na shule ya St Jude

–          Mwombaji awe Mtanzania mwenye Umri usio pungua Miaka 25

–          Mwombaji awe na ujuzi wa kuwakarimu watu na kufuata kanuni za Ajira

Vigezo na Masharti

Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu:

–          Aambatanishe barua ya maombi na Maelezo binafsi (CV)

–          Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Moshono Kampusi kabla au mnamo Jumatatu, tarehe  1 Julai 2024. Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.

–          TUTAWASILIANA NA WALE WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAHOJIANO!

ANGALIZO:

TAFADHALI KUWA MAKINI NA MATENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI.