Nafasi ya Kazi ya Udereva, Shule ya Sekondari Orkeeswa Arusha

Spread the love

NAFASI YA KAZI YA UDEREVA.

Shule ya Sekondari Orkeeswa Iliyopo Wilaya ya Monduli -Mkoa wa Arusha inatangaza nafasi ya kazi ya Udereva kwaajili ya kuendesha magari ya shule.

MUOMBAJI AWE NA VIGEZO VIFUATAVYO

1.Awe mtanzania 

2.Awe na Leseni Ya Udereva yenye sifa za kuendesha magari Binafsi na Abiria

3.Awe Tayari kuishi ndani ya wilaya ya Monduli karibu na kituo cha kazi

4.Awe na utayari wa kufanya shughuli nyingne tofauti na kuendesha magari wakati wa mchana

Wanawake watapewa kipaumbele hivyo waombaji wanawake wenye sifa wanasisitizwa kutuma maombi yao.

MAOMBI YATUMWE KUPITIA hr@orkeeswa.org au Fika shuleni na Barua yako ya Maombi

Maombi yatapokelewa kuanzia tarehe 12-28 March 2024.