Nafasi Za Kazi , St Lucia – Mlezi Wa Watoto

Spread the love

Nafasi Za Kazi , St Lucia – Mlezi Wa Watoto

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 MLEZI WA WATOTO 

(Malezi, Makuzi, Upishi na Usafi)

Shirika la St Lucia, Tumejikita kuboresha nyanja zote za ukuaji na maendeleo ya afya za walengwa wetu kupitia kituo chetu cha watoto yatima/Nursing-home, Huduma ya Majumbani kupitia wahudumu wetu kwenye jamii katika jamii zilizo katika mazingira hatarishi nchini Tanzania.

SIFA ZA MWOMBAJI.

Awe amehitimu Elimu ya Awali/Diploma, Makuzi na Malezi ya Watoto kwenye Vyuo rasmi vinavyotambulika na Serikali.

Awe na nidhamu na hofu ya Mungu. 

Awe anajituma bila kufuatiliwa na wepesi wa kufuata maagizo.

Awe na utayari wa kufanya kazi Night Shift . 

Awe na uwezo na uzoefu wa mapishi ya zaidi ya watu 8.

Awe na uzoefu wa kufanya usafi kwa kiwango cha hali ya juu.

Awe na uzoefu wa kuandika taarifa fupi na kwa undani.

Awe mbunifu na uzoefu wa kujiongeza kwenye utekelezaji wa majukumu anayopewa.

MAJUKUMU.

Malezi na makuzi ya watoto umri kwanzia miaka 2-18.

Kufanya usafi mdogo na usafi wa jumla.

Kuandaa chakula na kufuata Ratiba ya Kituo.

Kutoa Taarifa za kila siku kuhusiana na malezi ya watoto.

Kusimamia Store za vyakula na mahitaji ya watoto.

Kusimamia na Kushirikina katika shughuli za bustani za kituo. 

Kutimiza majukumu mengine ya malezi kama atakavyoagizwa.

Location: Arusha

Maombi/Maulizo yote yaelekezwe ukiambatanisha vivuli vya vyeti , CV na Barua ya maombi : recruitmentstlucia@gmail.com