Maelfu ya Vijana Waitwa Kwenye Usaili – Idara ya Uhamiaji / Immigration Services Department.

Idara ya Uhamiaji inawatangazia vijana wafuatao waliotuma maombi ya nafasi za Ajira kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kufika kwenye usaili utakaofanyika katika Ukumbi wa Café Theatre 1 & 2 Ndaki (Faculty) ya Biashara na Uchumi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) siku ya Jumamosi tarehe 28 Januari, 2023 saa 1:00 kamili asubuhi.

KUITWA KWENYE USAILI

Idara ya Uhamiaji inawatangazia vijana wafuatao waliotuma maombi ya nafasi za Ajira kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kufika kwenye usaili utakaofanyika katika Ukumbi wa Café Theatre 1 & 2 Ndaki (Faculty) ya Biashara na Uchumi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) siku ya Jumamosi tarehe 28 Januari, 2023 saa 1:00 kamili asubuhi.

Kwa wale waliotuma maombi kupitia Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kufika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja siku ya Jumamosi tarehe 28 Januari, 2023 saa 1:00 asubuhi.

Waombaji wote wanatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Kuzaliwa, Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Kidato cha Sita, Cheti cha Shahada, Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kutoka JKT/JKU, Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kalamu ya wino ya buluu, Vyeti vingine vya Kuhitimu Mafunzo katika fani mbalimbali ngazi ya Astashada na Stashahada.

Kwa waombaji ambao muundo wa fani zao unatakiwa kusajiliwa na Bodi za Taaluma, wanatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi kwa fani husika. Mara baada ya usaili wa awali kumalizika, Waombaji wa fani za Udereva, Ufundi wa Magari na TEHAMA wataendelea na Usaili kwa Vitendo siku inayofuata ya tarehe 29 Januari, 2023.

Aidha, wasailiwa wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili.

Soma Pia: Several New Job Vacancies at UNITEC Civil Consultants Ltd January, 2023

KUITWA KWENYE USAILI: TN17/01/2023

ZINGATIA:
• Kuvaa mavazi rasmi na nadhifu yenye heshima unapokuja kwenye usaili.
Atayevaa nguo za kubana/fupi, jeans, t-shirt, kaptula na tracksuit hataruhusiwa kuingia kwenye usaili.
• Mwombaji yeyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

  1. WANAOITWA KWENYE USAILI KUPITIA OFISI YA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI MAKAO MAKUU DODOMA, WATAKAOFANYA USAILI KATIKA UKUMBI WA CAFÉ THEATRE 1 & 2, CHUO KIKUU CHA DODOMA.

Maelfu ya Vijana Waitwa Kwenye Usaili – Idara ya Uhamiaji / Immigration Services Department – Kusoma Orodha nzima ya Majina, Tafadhali Bofya Kitufe kwenye linki hii ifuatayo , bofya neno ‘ Download ‘ hapo chini:-

Connect to Our Network of Sites For more Instant Opportunities Updates Like this!