Nafasi 12 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Pangani

Spread the love

Soma Hapa , Tangazo la Nafasi 12 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Pangani :-

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI

Unapojibu tafadhali taja:

Kumb Na: HWP/CS.10/36/141                                                                 20/05/2025

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani amepokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichotoa idhini ya utekelezaji wa nafasi za Ajira Mpya katika ikama ya mwaka wa fedha 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA. 97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi ya kazi katika nafasi zifuatazo:-

1.1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7

1.1.2  SIFA ZA MUOMBAJI

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.3 KAZI NA MAJUKUMU

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama ya gari

ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya magari.

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.

vi. Kufanya usafi wa gari.

vii. Kufanya kazi nyingine za fani yake akazopangiwa na Mkuu/Msimamizi wake wa kazi.

1.1.4 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

1.2.  MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5

1.2.1 SIFA ZA MUOMBAJI

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) na amehitimu Stashahada/Diploma ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa Dakika Moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile:- Word, Excel, Power Point, Internet, E-mail, na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.2.2 KAZI NA MAJUMKUMU

i.   Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri,

ii.  Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;

iii.  Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;

iv. Kupokea  majalada  na  kusambaza  kwa  maofisa  walio  katika  Divisheni, Vitengo na Sehemu zinazohusika;

v.  Kukusanya,   kutunza   na   kuyarejesha   majalada   na   nyaraka   sehemu zinazohusika;

vi. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

1.2.3  NGAZI YA MSHAHARA.

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

1.3.  MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.

➢  Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na umri usiopungua miaka 18

➢  Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa,

➢  Waombaji waambatanishe amelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye Anuani, Namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika,

➢  Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya Kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Ajira Portal,

➢  Testimonials  “Provision  Results”,  “Statement  of  Results”  Hati  ya Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVIKUBALIKI,

➢  Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika ukurasa wa Ajira Portal,

➢  Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE,

➢  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi,

➢  Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka wenye Kumb. Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010,

➢  Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria,

➢  Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02 Juni, 2025,

➢  MUHIMU:   Kumbuka   kuambatanisha   barua   yako   ya   maombi   ya   kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya barua hiyo ielekeze kwa:-

Mkurugenzi Mtendaji,

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, S. L. P. 89,

PANGANI.

➢  Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielekroniki wa Ajira (Recruitment

Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Secretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Imetolewa na;

Charles E. Fussi

MKURUGENZI MTENDAJI (W) PANGANI.

Jinsi ya Kutuma Maombi :-

Tuma Maombia Kupitia Viunganishi Vifuatavyo :-

POST: DEREVA DARAJA II – 7 POST
Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
Tuma Maombi Hapa

POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST
Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
Tuma Maombi

Soma Pia: – Nafasi ya Kazi , IRA AUTO SERVICES – Mshauri wa Huduma