TAMISEMI: TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE – TSP
Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu (Global Partnership for Education Teacher Support Programme – GPE – TSP) kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo ya kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea (engagement of volunteer teachers). Mradi huu unatangaza nafasi za kujitolea kwa walimu 694 wa Shule za Msingi watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa katika shule zenye uhitaji mkubwa zaidi kwa kuzingatia utaratibu wa kupanga walimu wa Shule za Msingi ‘Primary Teacher Allocation protocol (P – TAP)´ambao umeanishwa kwenye Andiko la Mradi huo wa GPE – TSP.
Hivyo, wahitimu kutoka Vyuo vya Ualimu na vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kujitolea katika Shule za Msingi mbalimbali kama zilivyoanishwa katika Mfumo wa ‘Online Teachers Application System (OTEAS)’ kuanzia tarehe 17 Mei – 30 Mei, 2025. Nafasi zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma).
1.0 TARATIBU ZA KUOMBA
Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2023.
2.0 SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI
Walimu wanaoomba kujitolea katika Shule za Msingi wanatakiwa kuwa na sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:
(i) Mwalimu Daraja la III A – Mwenye Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (Certificate in Primary Education);
(ii) Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Awali; na
(iii) Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Msingi.
3.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
(i) Awe raia wa Tanzania;
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 43;
(iii) Aambatishe nakala ya cheti cha: Kuzaliwa, Kidato cha nne au sita, na Mafunzo ya Fani ya Ualimu.
(iv) Awe tayari kufanya kazi katika Shule za Msingi zenye mahitaji makubwa zaidi ya walimu wa kujitolea zilizopo pembezoni;
(v) Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine;
(vi) Awe hajawahi kufukuzwa au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa makosa ya kiutumishi;
(vii) Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA);
(viii) Waombaji waambatishe nyaraka zote muhimu katika mfumo; na (ix) Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Kwa maelezo ya ziada kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi tafadhali kupitia: www.tamisemi.go.tz au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Mei, 2025 saa 05:59 usiku.
Tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo: www.tamisemi.go.tz.
Limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI,
Mji wa Serikali – Mtumba, S.L.P 1923,
41185 DODOMA.
17 Mei, 2025
See also: Nafasi Za Kuandikishwa Jeshini – JWTZ
TAMISEMI: TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE – TSP