Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yamezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Oktoba. Pamoja na kutangazwa matokeo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo katika kata, shehia, vijiji, mitaa na vitongoji.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi, idadi ya watu nchini Tanzania imefikia milioni 61,741,120, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza leo Jumatatu Oktoba 31, 2022 wakati akitoa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Tangu sensa ya mwisho ifanyike mwaka 2012, idadi ya watu ilikuwa 44,928,923, kumekuwa na ongezeko la zaidi ya Watanzania milioni 17.

Dar es Salaam ina 5,383,728 (8.7% ya Watanzania wote) wakati Mwanza ina 3,699,872 (6% ya Watanzania wote).

Idadi ya wanawake/wasichana nchini inafikia 31,687,990 ambayo ni 51% ya watu wote na idadi ya wanaume/wavulana ni 30,053,130 sawa na 49% ya watu wote.

Mikoa 10 yenye idadi ku zaidi ya watu nchini Tanzania.

  1. Dar es salaam : 5,383,728
  2. Mwanza 3,699,872
  3. Tabora : 3,391,679
  4. Morogoro : 3,197,104
  5. Dodoma : 3,085,625
  6. Kagera : 2,989,299
  7. Geita : 2,977,608
  8. Tanga : 2,615,597
  9. Kigoma: 2,470,967
  10. Mara : 2,372,015

Katika kutekeleza zoezi hilo, asilimia 98 ya wataalam waliohusika katika Sensa ya Watu na Makazi walikuwa ni Watanzania na wasomi wa ndani. Hayo yamesemwa leo Oktoba 31 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika uzinduzi wa taarifa ya sensa iliyofanyika mjini Dodoma.

Kwa takwimu rasmi zaidi za Matokeo hayo, bofya hapa.